3
KILA
KIINGIACHO MJINI…
1. Hivi
kweli kila kiingiacho, mjini ni halali?
Insi wakubali kila kinenwacho, ughaibuni
ni halali!
Maana waungama nacho, wakionapo
runingani.
2. Twakubali
kwani tunamacho, hata hatuoni mbali!
Ya ukweli na yasokificho, twabaini kila
hali,
Hii ni kweli kila kiingiacho, mjini ni
halali?
3. Kina
dada wafanyacho, miilini wameridhi na kukubali!
Wakwatuwa rangi zao na kubadili macho, ja
shetani au si kweli?
Watutumuwa maungo yao bila kificho, nasi
twakubali
Hii ni kweli kila kiingiacho, mjini ni
halali?
4. Kina
kaka wakata mikato, ya kila sampuli
Wafuasi kwa kila wakisikiacho, kwao ni
makubuli
Na wanafakhari watendacho, hata kama
sicho kwa staili
Au ndio kweli kila kiingiaho, mjini ni
halali!
5. Waduchu
wafungua macho, wayaona nayo wayanakili,
Wayadizaini, wayafuma na kuyaunda, mwisho,
huwa makali kama pilipili,
Waling’amua hawa kwa wakuu wakifanyacho, alimradi kisulisuli!
Ama kweli! Kila kiingiacho, mjini ni
halali!
6. Methali
ni zetu kweli twazikubali!
Kama fuata nyuki ili ule asali,
Au chovyachovya hatimae, humaliza buyu la
asali,
Ama kilio huanza mfiwa, ndipo wa mbali,
Na ile ya kivuli cha mvumo, hufunika
aliye mbali,
Pia ya mchele je! Mmoja, mapishi ni mbali mbali,
Ila nyengine si stahili, maana za umiza
matumbo kweli,
Kila kiingiacho mjini ni halali? Hii
yanipa mushikeli.
No comments:
Post a Comment