1.
TATA
1. Ta!
ta! Naanza kwa tata, kunena yanotokota,
Tata hili lasokota, vichanga linaambata
Wakuu nao wajuta, kwanini lawafuata
Tata hili tata gani? Bado linatukung’uta.
2. Juhudi
zinatusuta, kulitokomeza tata,
Kila leo tunateta, Bado limetufumbata,
Twapiga ngumi ukuta, aah! Twajikunyata,
Tata hili tata gani? Bado
linatukung’uta!
3. Sasa
mwishoni nasita, na tena najiokota.
Ta! Hili si la kugatwa, nanena tena nateta,
Ogopa sije kudota! Utakuja kuufyata,
Tata hili tata gani? Bado linatukung’uta.
No comments:
Post a Comment